KOCHA Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ni kupata ushindi wakiwa nyumbani.
Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 29 2024 na Machi 27 walifanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa leo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kocha huyo amesema mechi dhidi ya Al Ahly ni kubwa na wachezaji wanatambua namna ugumu ulivyo lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya.