MASHABIKI WA SIMBA WAPATA AJALI CHALINZE, PWANI

Basi dogo aina ya Costa lililobeba mashabiki wa Klabu ya Simba limepata ajali mapema alfajiri ya leo eneo la Vigwaza kata ya Wilaya ya Chalinze katika Mkoa wa Pwani.
Taarifa za awali zinasema mashabiki hao walikuwa wakitokea Tunduma kuja Dar es Salaam ambapo leo klabu hiyo ina mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Tayari Kamanda wa Polisi Pwani anaelekea eneo la tukio, taarifa zaidi kuhusu majeruhi zitawajia baadaye.