ANATUA USIKU MNENE MTU WA KAZI YANGA KUWAKABILI MAMELODI

KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns, uongozi wa Yanga umebainisha kwamba upo tayari kwa mchezo huo na wachezaji wake watawasili Tanzania muda wowote hata usiku wa manane kuwakabili wapinzani wao. Mchezo wa Yanga dhidi ya Mamelodi unatarajiwa kuwa Machi 30 2024 Uwanja wa Mkapa ikiwa ni hatua ya robo fainali.