RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema vifaa vya kiteknolojia kwa ajili ya kuwasaidia waamuzi (VAR), vitaanza kutumika rasmi katika mechi za Ligi Kuu Bara kuanzia msimu ujao.
Karia pia amekaribisha maoni ya kanuni ya kuzikata timu pointi ambazo wachezaji au mashabiki wake wataonekana kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina na kuingia uwanjani wakati mechi inaendelea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Karia amesema tayari wameshapokea nyaraka kutoka katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa ajili ya kupokea vifaa vya VAR, lakini kabla ya hapo kutakuwa na mafunzo kwa waamuzi ya namna ya kuvitumia.