UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly nguzo kubwa ya ushindi ni mashabiki jambo ambalo limewafanya waweke viingilio rafiki.
Ipo wazi kwamba Simba ina kibarua cha kusaka ushindi mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly hatua ya robo fainali Machi 29 2024 Uwanja wa Mkapa.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wanatambua ugumu uliopo kwenye mchezo huo lakini wapo tayari kutokana na maandalizi ambayo yanaendelea kufanyika.
Kuhusu viingilio itakuwa namna hii:-“Viingilio vya mchezo ni;
Mzunguko – Tsh. 5,000
Machungwa – Tsh. 10,000
VIP C – Tsh. 20,000
VIP B – Tsh. 30,000
VIP A – Tsh. 40,000
Platinum – Tsh. 200,000
Tanzanite – Tsh. 250,000