MWAMBA Pacome Zouzoua anasumbuliwa na maumivu ya goti alipata maumivu mchezo wa Mzizima Dabi.
Kuna hatihati kwa nyota hawa kuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Khalid Aucho alikosekana Mzizima Dabi anasumbuliwa na goti, Zawadi Mauya naye hayupo fiti huku Attohoula Yao aliumia kwenye nyama za paja na Kibwana Shomari anasumbuliwa na enka.
Kituo kinachofuata kwa Yanga ni dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amewekà wazi kuwa hakuna cha kuhofia daima mbele nyuma mwiko.
“Benchi la ufundi linasubiri ripoti kutoka kwa madaktari kujua hali zao zipoje lakini hatupaswi kuwa na hofu,”.