>

SIMBA WAIVUTIA KASI AL AHLY

WAKIWA na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, Waarabu wa Misri uongozi wa Simba umebainisha kuwa kambi yao itakuwa Zanzibar kwa maandalizi.

Timu hiyo inaiwakilisha Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wao wa hatua ya robo fainali unatarajiwa kuchezwa Machi 29 Uwanja wa Mkapa.

Mshindi kwenye mchezo wa kwanza atakuwa ametanguliza mguu mmoja hatua ya nusu fainali ambayo itaamuliwa kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza itakayochezwa Misri.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye kambi maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrka dhidi ya Al Ahly.

“Tutakuwa na mchezo dhidi ya Al Ahly ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika tunahitaji kuwa na utulivu mkubwa kuelekea mchezo huo na malengo ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri.

“Kambi ya Zanzibar hii itampa muda mwalimu kuwafundisha wachezaji kwa utulivu na kuwa tayari kuelekea mchezo wetu dhidi ya Al Ahly, inawezekana kupata matokeo na muda ni sasa kwa ajili ya maandalizi hayo,”.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka Machi 19 kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi ya mudainayotarajiwa kuwa ni muda wa siku 7 mpaka 8