WASHINDI wa tuzo ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na Beki ya Taifa NBC kwa Februari wamekabidhiwa tuzo zao huku makubwa yakiahidiwa.
Yote hayo yalifanyika Machi 17 2024 ambapo NBC ilikabidhi zawadi ya pesa na tuzo kwa kocha bora wa ligi hiyo wa mwezi Februari.
Ni Miguel Gamond kutoka Klabu ya Yanga alitwaa tuzo ya kocha bora ndani ya mwezi Februari.
Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika dakika chache tu kabla ya mchezo wa Azam FC dhidi ya Yanga SC kuanza ambapo alishuhudiwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya NBC, David Raymond akikabidhi tuzo pamoja na mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kocha Gamondi.