MATAJIRI wa Dar, Azam FC mkali wao wa kucheka na nyavu ni Feisal Salum akiwa kafunga jumla ya mabao 12 kati 45 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya tatu na pointi 44 baada ya kucheza mechi 20.
Yusuph Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa maandalizi yamekamilika kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga.
“Tumefanya maandalizi kamili kwa ajili a mchezo wetu dhidi ya Yanga na tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi hilo lipo wazi.
“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo itakuwa ni sehemu ya kuona namna gani tunafanya vizuri na kupata ushindi hivyo mashabiki wajitokeze kwa ajili ya kuhushudia burudani,”.
Ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-2 Azam FC.
Machi 17 Mzizima Dabi, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa wababe hao kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90.