WAPINZANI wa Yanga kwenye hatua ya robo fainali, Mamelod Sundowns wamebainisha kwamba wanatambua uimara wa Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika jambo ambalo linawafanya wajiandae kwa umakini.
Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Mamelod kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni mara ya kwanza kwa Yanga kutinga kwenye hatua hiyo.
Rhulani Mokwena Kocha Mkuu wa Mamelodi kuelekea mchezo wa hatua ya robo fainali amebainisha kwamba ambacho wanakifanya kwa sasa ni maandalizi mazuri.
“Natambua kuhusu wapinzani wetu Yanga na kocha Miguel Gamondi ni kocha mzuri ambaye amekuwa akipata matokeo mazuri hivyo tunafanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu.
“Ni lazima ujiandae mentally na tutafanya hivyo kwasababu mashabiki wana matarajio makubwa juu yetu na hatupaswi kuwaangusha kabisa.
“Yanga ni timu nzuri na imetengeneza historia yake kwenye hii michuano ya CAF champions League mfano mwaka jana walifika hadi fainali ya Confederation lakini pia walishinda ligi hivyo ni timu nzuri,”.
Mchezo wa mkondo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 29-31 Uwanja wa Mkapa.