UKUTA WA SIMBA NGOMA NI NZITO

BAADA ya kucheza mechi 18 za Ligi Kuu Bara na kuruhusu mabao 18 benchi la ufundi la Simba limebainisha kuwa watafanyia kazi makosa yanayotokea kwenye mechi zao katika uwanja wa mazoezi.

Ngoma ni nzito kwa ukuta wa Simba katika kutoruhusu mabao ya kufungwa kwenye mechi za ligi ambapo kwenye mechi tatu mfululizo imeshuhudia ikifungwa jumla ya mabao manne.

Mechi hizo ilikuwa Simba 1-2 Tanzania Prisons mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Coastal Union 1-2 Simba mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Simba 3-1 Singida Fountain Gate.

Wakati ukuta ukiruhusu mabao manne kwenye mechi hizo mfululizo ni mabao sita yamefungwa na safu ya ushambuliaji ya Simba huku mwamba Fred Michael akifunga mabao mawil kwenye mechi mbili mfululizo ilikuwa dhidi ya Coasta Union na Singida Fountain Gate.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa watafanyia kazi makosa yanayotokea kwenye safu ya ulinzi ili kutoruhusu mabao kwenye mechi zao.

“Ushindani ni mkubwa na kuna makosa ambayo yanatokea ikiwa kwenye safu ya ulinzi kuruhusu mabao ambacho tunakifanya ni kufanyia maboresho hasa kwenye eneo la uwanja wa mazoezi,”.

Simba leo ina kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.