NO PACOME NO PROBLEM, 10 SIMBA WAACHWA

UNAWEZA kusema hivyo No Pacome No Problem kwa mabingwa watetezi Yanga kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Namungo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa umesoma Namungo 1-3 Yanga ambapo katika dakika 45 za mwanzo hakuna timu iliyoruhusu bao kuokotwa kwenye nyavu zake.

Kipindi cha pili yuleyule aliwafunga Namungo Uwanja wa Azam Complex, Mudathir Yahya alifungua pazia la ufungaji dakika ya 46 kisha kamba ya pili ikafungwa na Clement Mzize dakika ya 57 Aziz KI dakika ya 62 akafunga bao la tatu.

Bao la Namungo ilikuwa ni la kujifunga kwa beki Bacca dakika ya 69 akiwa kwenye harakati za kuokoa hatari.

Ushindi huo unaifanya Yanga ambayo haikuwa na Pacome,Djigui Diarra,Khalid Aucho kwenye mchezo wa leo kufikisha pointi 46 wakiwa namba moja wakiwa tofauti ya pointi 10 na watani zao wa jadi Simba wenye pointi 36.