AHMED ALLY: KIPIGO CHA TANZANIA PRISONS KISITUVURUGE SIMBA

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wanapaswa kushikama na kuendelea kuisapoti timu yao na wachezaji wao licha ya kupoteza mchezo uliopita.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Tanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho Jumamosi katika Dimba la Mkwakwani huku Mnyama akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa kipigo cha bao 2-1.

“Matokeo ya Prison mimi mwenyewe nimeumia sana, nilikuwa kwenye hali mbaya mno ila sikulia. Nimesikitika, mechi ilikuwa ngumu ile. Hata nikilia hakuna shida kwa sababu naililia simba yangu lakini sina muda wa kulia.

“Haya ni maumivu yetu sote asijitokeze mtu akajimilikisha maumivu kuwa ni yake peke yake kwa sababu haya ni maumivu yetu sote. Ukitumia muda mwingi kutafuta mchawi unapoteza focus ya kujiandaa na mchezo ujao.

“Mechi ya Coastal ni ngumu vibaya mno, wale jamaa sio wa kawaida, wana hatari sana. Lazima tushikamane, la sivyo tutapoteza mchezo wa pili mfululizo na tutaanza kukimbiana hapa,” amesema Ahmed Ally.
spoti pesa below post