Meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti (64) anakabiliwa na kifungo cha takribani miaka mitano jela baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya ulaghai wa kodi nchini Hispania.
Waendesha Mashtaka wa Serikali wamemtuhumu Kocha huyo mwenye asili ya Italia kwa kutumia mfumo wenye kuchanganya chini ya Makampuni ya shell ili kuficha sehemu kadhaa za mapato yake.
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea na Everton anatuhumiwa kwa makosa mawili ya ulaghai wa kodi mwaka 2014 na 2015.
Hukumu ya makosa hayo huwa ni kifungo cha miaka hadi minne na miezi tisa jela.
Ancelotti ambaye ni mmoja wa makocha wenye mafanikio makubwa katika soka anatuhumiwa kulaghai kiasi cha euro Milioni 1.
Kwa mujibu wa waendesha Mashtaka, katika kipindi hicho, Meneja huyo aliripoti kipato chake cha Real Madrid tu na si kutoka kwenye vyanzo vingine vya mapato.