LIGI KUU BARA: SIMBA 1-2 TANZANIA PRISONS

FT: Mchezo wa ligi

Simba 1-2 Tanzania Prisons

Samson Mbagula goal dk 45, 62.

Goal kwa Simba ni Fabrince Ngoma dk 89.

AISHI Manula atajilaumu mwenyewe kwa kukaa kwa sekunde kadhaa akiwa langoni huku mpira ukiwa unaelekea langoni mwake na kumpa nafasi mpigaji kufunga kipindi cha kwanza.

Samson Mbangula alitumia makosa ya Simba kuwa wengi eneo la kushambulia lango lao wakafanya shambulizi la kushtukiza lililowapa bao la uongozi.

Mzunguko wa pili mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons ni Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Simba ipo mikononi mwa Wajelajela ambao wanacheza mpira wa pasi ndefu tofauti na Simba wanaocheza mpira wa pasi fupi jambo linalowafanya waingie kwenye mfumo wa Prisons.

Amos Yona kipa wa Tanzania Prisons katika dakika 45 za mwanzo ni shujaa kwa kuokoa hatari zaidi ya mbili ikiwemo moja waliyojichanganya na beki wake lakini Bababacr Sarr alikosa kufunga akiwa ndani ya 18.