DUBE ANASEPA AZAM FC KUIBUKIA MITAA YA KARIAKOO

MUUAJI anayetabasamu Prince Dube ameomba kuondoka ndani ya kikosi cha Azam FC baada ya kuandika barua ya kuomba kuvunja mkataba wake.

Dube ambaye amekuwa akiwatesa wababe wa Kariakoo hasa Simba amekuwa na zali la kuwafunga kila anapokutana nao kwenye mechi za ushindani amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo kati ya Simba na Yanga.

Ikiwa itakuwa hivyo basi nyota huyo atakuwa huru kujiunga bure kwenye moja ya timu hizo ama atakuwa na dili jingine nje ya Bongo.

Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao ulisomaSimba 1-1 Azam FC na bao la Azam FC lilifungwa na Dube dakika ya 14 akitumia pasi ya Pascal Mshindo.

Uongozi wa Azam FC umebainisha kuwa mshambuliaji huyo yupo huru kuondoka ikiwa atakamilisha taratibu zilizopo kwenye mkataba.

Miongoni mwa masharti ambayo amepewa kwa mujibu wa mkataba ikiwemo kulipa Dola za Kimarekani 300,000/

Zakaria Thabit Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Azam FC amesema kuwa mshambuliaji huyo yupo huru kuondoka.