AZAM FC WANA JAMBO LAO

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Yusuph Dabo amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa watazidi kupambana kwa kuwa wana jambo lao kila mchezouliopo mbele yao wakihitaji kufanya vizuri.

Azam FC kwenye mechi mbili mfululizo iliambulia sare ilikuwa dhidi ya Tabora United na Tanzania Prisons.

“Tupo imara kwenye mechi ambazo tunacheza na malengo yetu ni kuona kwamba tunakuwa bora kwa kuwa makosa ambayo yanafanyika tunafanyia kazi. Kila mchezo unakuwa na mbinu.

“Ninafurahia namna wachezaji wanavyojituma kwenye kutimiza majukumu bado tunaendelea kufanyia kazi makosa na yale mazuri tunafanyia maboresho kwa mechi zinazofuata”.

Azam FC pointi 40 baada kucheza mechi 18 ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi tofauti ya pointi tatu na vinara Yanga wenye pointi 43.

Mchezo wake uliopita ilikuwa dhidi ya Singida Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba iliposhinda kwa bao 1-0 likifungwa na Kipre Junior dakika ya 53 kweye mchezo huo.