YANGA NDANI YA MORO KUIKABILI KMC

VINARA wa Ligi Kuu Bara Yanga wapo ndani ya Morogoro ambapo waliwasili mapema Februari 15 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi.

Ni pointi 40 wanazo kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 15 mchezo wao wa kukamilisha mzunguko wa kwanza ilikuwa Uwanja wa Sokoine ubao uliposoma Prisons 1-2 Yanga wakakomba pointi tatu jumlajumla.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya KMC unatarajiwa kuchezwa Februari 17 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo kila timu inahitaji pointi tatu muhimu.

Baada ya kuwasili walipata muda wa kufanya mazoezi ya kuweka miili sawa chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamond.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa mpango mkubwa ni kuanza mzunguko wa pili kwa ushindi ili kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kutwaa ubingwa.

Miongoni mwa wachezaji waliopo Moro ni pamoja na Aziz KI, Aboutwalib Mshery, Maxi Nzengeli, Khalid Aucho.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo uliopita yalifungwa na Clement Mzize pamoja na Pacome ambaye alitoa pia pasi ya bao dakika ya 7 kwa Mzize.