GEITA GOLD YAPOTEZA MBELE YA SIMBA

KWENYE mechi mbili mfululizo Uwanja wa CCM Kirumba, Simba inaambulia pointi dakika za lala salama katikà mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Walianza Februari 9 ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC, bao lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 90 Simba wakakomba pointi moja.

Februari 12 ubao umesoma Geita Gold 0-1 Simba bao likifungwa na Babacar Sarr dakika ya 81 akiwa ndani ya 18.

Simba inafikisha pointi 33 ikiwa tofauti ya pointi Saba na vinara Yanga wenye pointi 40.

Simba inapanda nafasi moja kutoka ilipokuwa awali ile ya tatu  inayokuwa mikononi mwa Azam FC.