Klabu ya Yanga leo Feburari 6, 2024 imesani mkataba wa miaka miwili na Hospitali ya Aga Khan kwa ajili wachezaji kufanyiwa vipimo vya afya bure na Wanachama wetu kupata punguzo kubwa la bei wanapokwenda kutibiwa kwenye Hospitali ya Aga Khan wakiwa na kadi zao za Uanachama.
“Lengo la klabu ya Yanga kuingia mahusiano na Hospitali ya Aga Khan ni kuwafikia wanachama wetu katika huduma za afya kwa bei pungufu. Tunafahamu kuwa kuna watu wanafikra kuwa Hospital ya Agha Khan ni hospitali ya bei ghali lakini niwatoe wasiwasi mtakapokwenda kwenye matawi ya Agha Khan maeneo mlioyopo kwa kutumia kadi za uanachama za Yanga SC”
“Mwanachama wa Yanga mwenye kadi ya Uanachama ambayo ni kadi hai atapata punguzo la gharama baada ya kutibiwa katika hospitali za Aga Khan” amesema Rais Yanga, Injinia Hersi Said
“Tunajivunia kuingia mkataba wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa klabu yenye historia kubwa sana Tanzania. Sisi kama Aga Khan tumekuwa na heshima kubwa ya kutoa huduma za afya kwa jamii, lakini mahusiano haya yanatupatia heshima ya kipekee. Tunawajibu mkubwa kuhakikisha tunautumikia mkataba huu kwa juhudi kubwa” Sisawo Konteh – Mtendaji Mkuu Aga Khan Hospital