YANGA KUIKABILI DODOMA JIJI

 BAADA ya kuambulia sare mchezo wao wa kwanza ndani ya Februari 2 2024 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga kesho wanashuka kwa mara nyingine tena uwanjani.

Kesho Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Yanga ilikomba pointi moja ugenini Uwanja wa Kaitaba ikiwa ni sare yake ya kwanza ndani ya msimu wa 2023/24.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha kwanza ni pamoja na Metacha Mnata ambaye ni mlinda mlango,Khalid Aucho, Pacome na Maxi Nzengeli.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa kazi kubwa kwenye mechi zao ambazo wanacheza ni kusaka pointi tatu.

“Kwenye mechi ambazo tunacheza kikubwa tunahitaji kupata pointi tatu muhimu, tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa nasi tutajitahidi kupata matokeo,”.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 12 ushindi ni mechi 10 imepoteza mchezo mmoja na sare mchezo mmoja ina pointi 31.