MALI NDO BASI TENA AFCON

LICHA ya kuanza kutangulia kufunga bado hawajatusua kutinga hatua ya nusu fainali hivyo Mali kwa 2023 kutwaa taji hilo ndo basi tena mpaka wakati ujao.

Mali ilipoteza kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo imetinga hatua ya nusu fainali Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) baada ya kuiondosha Mali kwa mabao 2-1.

Mchezo huo ulimalizika dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 yakifungwa na kiungo, Dorgeles Nene kwa Mali huku mshambuliaji, Simon Adingra akiisawazishia Ivory Coast kabla ya kwenda 30 za nyongeza ndipo, Oumar Diakite akawafungia wenyeji hao bao la ushindi dakika ya 120.

Ivory Coast ililazimika kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki wake, Odilon Kossounou kupewa kadi nyekundu dakika ya 43 kipindi cha kwanza.

Ipo wazi kuwa Ivory Coastl  walifuzu hatua ya 16 bora wakiwa ni ‘best looser’ kisha kuiondosha Senegal na kutinga robo fainali kabla ya hii leo kuwaondosha pia Mali.

Ivory Coast itakutana na DR Congo katika mchezo wa nusu fainali ambayo timu hiyo yupo Fiston Mayele na Henock Inonga wanaoitambua vema Ligi Kuu Bara ya Tanzania.