UONGOZI wa Tabora United umeweka wazi kuwa unajivunia uwepo wa nyota wao John Noble ambaye ni kipa namba moja wa timu hiyo.
Tabora United ni miongoni mwa timu ambazo zimepanda daraja zikiwa zinapambana kufanya vizuri kwenye ligi.
Ofisa Habari wa Tabora United, Chritina Mwagala ameweka wazi kuwa wachezaji wao wanafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwa kwenye ubora kitaifa.
Mwagala amesema:” Tupo imara kwenye mechi ambazo tunacheza na tunatambua ushindani mkubwa ambapo tuna kipa ambaye ni kinara kwa makipa ambao hawajafungwa kwenye mechi nyingi.
“Noble ndiye kinara wa hati safi (cleansheet) kwenye Ligi Kuu Bara tunaamini kwamba ataendelea kufanya vizuri kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,”.