YANGA YATOA ANGALIZO KWA WAPINZANI WAO KISA MSHAMBULIAJI MPYA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa usajili wa mshambuliaji wao mpya Guede utawaongezea kasi kwenye suala la kufunga huku wapinzani wao wakionywa kutokana na uwezo wa mshambuliaji huyo mwenye uzoefu wa kucheza mechi za ushindani. Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo ilimtambulisha Guede raia wa Ivory Coast kuwa miongoni mwa nyota wao wapya huku mwamba Hafiz Konkoni akitolewa kwa mkopo.