SITA HAWATAKUWA NDANI YA SINGIDA FOUNTAIN GATE

MASTAA sita wamekutanana mkono wa asante ndani ya kikosi cha Singida Fountain Gate inayotumia Uwanja wa Liti kwa mechi zake za nyumbani.

Timu hiyo ilishiriki Mapinduzi 2024 na ikagotea hatua ya nusu fainali ilipofungashiwa virago na Simba kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Miongoni mwa nyota ambao hawatakuwa ndani ya Singida Fountain Gate kwa msimu wa 2023/24 kwenye mechi zinazofuata ni pamoja na Marouf Tchakei, Duke Abuya  mlinda mlango Khomeiny Aboubakar Khomeiny.

Mbali na hao ambao inatajwa kuwa wanaweza kuibukia Ihefu FC pia beki kisiki Joash Onyango,  Mussa Ibrahi na kiraka Gadiel Michael naye amekutana na Thank You.

 Gadiel amepewa baraka na Singida Fountain Gate ambapo anakwenda kujiunga na moja ya timu Afrika Kusini kwa ajili ya changamoto mpya inaitwa Cape Town Spurs .