WAKATI miamba wawili Jean Baleke na Moses Phiri wakikutana na Thank You ndani ya Simba wanatajwa kuwa sababu ya Abdelhak Benchikha kocha wa Simba kuongeza nafasi ya kufungashiwa virago ikiwa nyota wapya watashindwa kufanya vizuri.
Phiri kwenye ligi katupia mabao matatu huku Baleke akitupia mabao 8 katika Mapinduzi 2024 kila mmoja alitupia bao mojamoja.
Wengine ambao wamepewa Thank You Simba ni Shaban Chilunda, Mohamed Mussa, Jimmyson Mwanuke na Nassoro Kapama.
Ni Fredy Michael, Pa Omary Jobe hawa wanatarajiwa kubeba mikoba ya miamba hiyo miwili. Hivyo ikiwa ni pendekezo la kocha kwa maamuzi haya kwa wachezaji waliokuwa wakionyesha angalau uwezo wa kutumia nafasi walizopata kuna ugumu kwa kocha huyo kuendelea kubaki ndani ya Simba.