KOMBE la Mataifa Afrika, (AFCON) uhondo unazidi kuwa mkali kwa kuwa kila timu inaonyesha uwezo wake ndani ya dakika 90 kusaka ushindi.
Miongoni mwa timu zilizoanza kwa ushindi ni Mali ambapo kipa aliyeanza langoni ni Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja wa Yanga.
Katika mchezo uliochezwa Januari 16 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mali 2-0 Afrika Kusini.
Mabao yalifungwa na Hamari Traore dakika ya 60 Lassine Sinayoko dakika ya 66.
Januari 17 ni mchezo wa kwanza kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa dhid ya Morocco saa 2:00 usiku.