Mlandege ni mabingwa wa Mapinduzi kwa mara ya pili walianza kutwaa mbele ya Singida Fountain Gate 2023 na 2024 mbele ya Simba.
Akandwanao amefunga bao kipindi cha pili akiwa ndani ya 18 akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Simba kwenye kukaba mali
Kipindi cha pili
Uwanja Amaan Complex ngoma ni nzito kwa timu zote mbili ambazo zinapambania taji la Mapinduzi 2024.
Katika dakika 45 za mwanzo ubao unasoma Mlandege 0-0 Simba huku kila timu ikiingia na mpango kazi wake.
Kwa upande wa Mlandege wameingia na mbinu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza huku Simba wakiwatumia viungo kufanya mashambulizi mara kwa mara langoni mwa Mlandege.
Umakini wa mlinda mlango wa Mlandege unawapa ugumu Simba kama ilivyo Ayoub Lakred ambaye kosa lake alilofanya katika kutoa pasi yeye mwenyewe alilisahisha.