MSHAMBULIAJI HUYU YANGA ANASEPA

INAELEZWA kuwa nyota wa Yanga, Cripin Ngush ambaye ni mshambuliaji atakuwa ndani ya uzi wa Coastal Union ya Tanga kwenye kupambania nafasi kikosi cha kwanza.

Ipo wazi kwamba mshambuliaji huyo mzawa ambaye aliibuka ndani ya Yanga akitokea Mbeya Kwanza hana nafasi kikosi cha kwanza.

Alipata zali la kuanza kikosi cha kwanza kwenye baadhi ya mechi za Kombe la Mapinduzi 2024 alipofunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri kabla ya timu hiyo ugotea hatua ya robo fainali ikifungashiwa virago na APR FC ya Rwanda.

Anatajwa kwamba baada ya msimu kumalizika atarejea ndani ya Yanga akiwa ni mwenye uwezo mwingine na kupata nafasi kikosi cha kwanza.

Yanga ipo chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambaye hivi karibuni aliweka wazi kuwa kazi kubwa ya mchezaji ni kupata nafasi na kuonyesha uwezo wake uwanjani.