NYOTA HAWA WANA BALAA WAKIWA UWANJANI

NDANI ya Ligi Kuu Bara kuna miamba ambao wana juhudi kwa kuwa namba moja kwenye rekodi tofautitofauti. Ni Aziz KI huyu anakipiga Yanga ni namba moja kwa watupiaji wa mabao akiwa nayo 10 na ni kinara kwa watupiaji wakitumia mguu wa kushoto na mkali wa mapigo huru. Saido Ntibanzokiza ni mkali wa penalti yupo zake Simba huku Jean Baleke mkali wa kutumia mguu wa kulia.