HAALAND ANAIRUDISHA DUNIA NYUMA

Wakati wengi wakiamini dunia inaenda mbele na mambo yamebadilika lakini mtu mmoja ameweza kufanikiwa kuirudisha dunia nyuma, Huku pia dunia ikikubali kuishi ndani ya dunia ya mtu huyo sio mwingine ni Earling Haaland.

Katika ulimwengu ambao wengi wanaamini mshambuliaji anapaswa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja kama kufunga, uwezo wa kuiunganisha timu katika eneo la mbele, Hapo ndipo alipoibuka kijana kutoka Norway mzaliwa wa Leeds West Yorkshire na kuirudisha dunia nyuma.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako. utakua ni mchezo wa pili kukutanisha vilabu hivyo msimu huu baada ya kukutana

Tunasema Haaland kairudisha dunia nyuma na dunia imekubali kwenda nae sawa kwakua mshambuliaji huyo ni aina ya washambuliaji wa zamani kutokana na staili yake ya uchezaji akicheza kama baadhi ya washambuliaji wa miaka ya 2000’s na 1990’s.

Staa huyo wa klabu ya Manchester City ni mshambuliaji ambaye anasubiri zaidi mipira ndanmi ya eneo la hatari na hana uwezo wa kucheza kwa kuunganisha timu kuanzia chini kama wafanyavyo washambuliaji wengi wa kizazi hichi.

Jambo la kushangaza ni kua licha ya mshambuliaji huyo kutokua na uwezo wa kuunganisha na kuchezesha timu katika eneo la mbele uwanjani amefanikiwa kukonga nyoyo za makocha wake, Huku siri kubwa ikiwa ni namna ambavyo amekua na uwezo kutumia nafasi ambazo zimekua zikipatikana na kumfanya kua mshambuliaji hatari zaidi duniani kwasasa.

Earling Haaland amekua mchezaji pekee ambaye amemfanya kocha kiburi Pep Guardiola kukubali kuvunja misimamo yake, Kwani Guardiola ni muumini wa washambuliaji wakisasa na wenye uwezo wa kushiriki mchezo kwa kiwango kikubwa na ndio sababu ya kumuondoa Sergio Kun Aguero ndani ya Man City lakini kwa Haaland amenyoosha mikono.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee

ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia na uweke mkeka wako.