CHELSEA WAANZA MWAKA KIBABE, WASHINDA MECHI TAU

Klabu ya Chelsea wanakuja vizuri siku za karibuni kutokana na kushinda michezo kadhaa mfululizo jambo ambalo limekua nadra kwa klabu hiyo sio msimu huu tu bali kwa misimu miwili ya hivi karibuni.

Unaweza kusema Chelsea wameanza kuja taratibu kutokana na hali yao katika ligi kuu ya Uingereza msimu, Hivo wao kupata matokeo ya ushindi mfululizo katika michezo yao ya hivi karibuni imeonesha utofauti na imani kuanza kurejea kwa matajiri hao kutoka jijini London.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.

Licha kuwepo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza lakini haiondoi kua matajiri hao wa jiji la London wameanza kuonesha mabadiliko katika michezo yao, Hivo kutoa matumaini makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Moja ya matatizo ambayo yalikua yanaiandama klabu ya Chelsea ni pamoja na majeraha ambayo yamekua yakiwandama baadhi ya wachezaji wao wa kikosi cha kwanza, Ikielezwa ni moja ya sababu zilizofanya klabu hiyo kutokufanya vizuri.

Klabu ya Chelsea mpaka sasa imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao Cup na leo watashuka dimbani kumenyana na klabu ya Middlesbrough, Hii imechangiwa na michezo yao mitatu ya hivi karibuni ambayo wamecheza.

Vijana wa kocha Pochettino ni wazi wameanza kuibua matumaini kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao ni kama walianza kuikatia tamaa timu yao, Lakini hivi karibuni klabu hiyo imeonesha mabadiliko makubwa katika michezo yake ambayo imecheza.

Kilichobakia kwa klabu ya Chelsea kwasasa ni muendelezo wa ambacho imekua ikikifanya hivi karibuni ili kuweza kurejea kwenye ubora wao ambao wamekua nao kwa takribani misimu mitatu iliyopita ambayo walifanikiwa kutwaa taji la ulaya.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee

ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia na uweke mkeka wako.