MLANDEGE WANAWAVUTIA KASI SIMBA NA SINGIDA FOUNTAIN GATE

MLANDEGE imetinga kwa mara ya pili mfululizo fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufanya hivyo 2023 na hatimaye kwa mara nyingine ni 2024.

Katika hatua ya nusu fainali baada ya dakika 90 ilikuwa Mlandege 0-0 APR hali iliyopelekea mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penalti.
Ilikuwa Mlandege 4-2 APR huku mpigaji wa kwanza kwa APR nahodha Shiboub mkwaju wake ukiokolewa na kipa wa Mlandege aliyekuwa kwenye ubora wake.
Ni mabingwa watetezi Mlandege wanasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya Januari 10 2024, Simba v Singida Fountain Gate ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwenye mchezo huo kadi mbili nyekundu zilitolewa moja kwa mchezaji wa APR na moja kwa mchezaji wa Mlandege ikiwa ni Masoud Juma na Nyigena Clement wa APR dakika ya 88.

Mabingwa watetezi Mlandege wanawavutia kasi Singida Fountain Gate ama Simba ambao watakuwa kwenye msako wa mshindi atakayefuata kwenye fainali.