KLABU bora Bongo Azam FC kwa mara nyingine tena wamekwama kufurukuta mbele ya Singida Fountain Gate katika Kombe la Mapinduzi kwa kuwa ni mara ya pili kufungashiwa virago na timu hiyo.
Ikumbukwe kwamba Januari 8 2023 ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC 1-4 Singida Fountain Gate katika hatua ya robo fainali zama hizo ilikuwa inaitwa Singida United.
Kwa mara nyingine tena Januari 8 ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC 1-2 Singida Fountain Gate.
Ni Allasane Diao mwili jumba alifunga bao dakika ya 45+4 kisha yale ya Singida Fountain yalifungwa na Elvis Rupia dakika ya 62 na lile la ushindi lilifungwa na Habib Kyombo.
Nusu fainali itakuwa Singida Fountain Gate dhidi ya Simba, Januari 10 na leo Januari 9 ni Mlandege v APR ya Rwanda.