MWAMBA Ladack Chasambi ambaye ni kiungo ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba ikiwa ni ingizo jipya.
Timu hiyo ya Simba chini ya Abdelhackh Benchika inatarajiwa kucheza mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Jamhuri kwenye Kombe la Mapinduzi leo Januari 8 2024.
Ikiwa itapoteza kwenye mchezo wa leo itafungashiwa virago na kugotea mwisho kwenye mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa watani zao wa jadi Yanga ambao Januari 7 walimaliza mwendo kwa kushuhudia ubao ukisoma Yanga 1-3 APR.Simba kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram imemtambulisha kiungo huyo kwa kusema, “Karibu Ladack Chasambi,”.
Nyota mwingine ambaye alitambulishwa ndani ya Simba ni Saleh Karabaka, Babacarr Sarr raia wa Senegal ambapo wote hawa ni viungo.