SINGIDA FOUNTAIN GATE YATUMA UJUMBE HUU AZAM FC

NIZAR Khalfan, kocha msaidizi wa Singida Fountain Gate ameweka wazi kuwa hawatakubali kupoteza kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Azam FC, unaotarajiwa kuchezwa leo Januari 8 2024.

Ikumbukwe kwamba mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo ilikuwa ni robo fainali kwa wababe hawa wanaokutana kwa mara nyingine ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC 1-4 Singida Fountain Gate.

Mabao ya Singida Fountain Gate yalifungwa na Francy Kazadi huku lile la Azam FC likifungwa na Abdul Suleiman, (Sopu) ambaye hajawa na nafasi kikosi cha kwanza kwenye mechi za hivi karibu.

Khalfan ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wataingia kwa nidhamu ili kupata matokeo kwenye mchezo huo.

“Tunatambua mchezo utakuwa mgumu lakini hatutakubali kupoteza mchezo wetu dhidi ya Azam FC. Tunawaheshimu na tunajua kwamba wamekuwa kwenye mwendo mzuri katika mechi wanazocheza,”.