AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye mechi zote ambazo watacheza.
Kwa sasa Simba inashiriki Kombe la Mapinduzi ambapo imetinga hatua ya robo fainali ikivunja rekodi yake mbovu ya kukwama kufika katika hatua hiyo 2023.
Ni mchezo dhidi ya Jamhuri itakuwa katika hatua ya robo fainali ambapo unatarajiwa kuchezwa Januri 8 2024 ikiwa watapata ushindi watakata tiketi kutinga hatua ya nusu fainali.
Ally amesema:”Wachezaji wanatambua kazi iliyopo ni kutafuta ushindi na tunaamini itakuwa hivyo mpaka tutakapokamilisha malengo, ushindani ni mkubwa nasi tunaendelea kufanya maandalizi mazuri,”.