WACHEZAJI MUHIMU KUCHEZA KWA UMAKINI

WAKATI uliopo kwa sasa kwa timu shiriki kwenye Kombe la Mapinduzi 2024 ni kuendelea kutimiza majukumu yao wanayopewa. Ipo wazi kwamba kila timu inapenda kupata matokeo ndani ya dakika 90.

Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba timu inakosa matokeo hivyo jambo la muhimu ni kufanya kazi kwa umakini kwenye mechi zote.

Wachezaji ni muhimu kuongeza umakini katika kucheza uwanjani ili kuwalinda wachezaji wengine wasipate maumivu kwa kuwa bado kuna mechi za kucheza.

Kuumizana kwenye mechi ambazo zinaendelea kwa makusudi inapunguza kasi ya mchezaji atakayepata maumivu kufikia malengo yake.

Nguvu kutumika uwanjani huwezi kukwepa lakini kuna nafasi ya kulindana kwenye kila mchezo ambao unachezwa uwanjani. Vita kuwa ya maumivu kwenye uwanja hilo sio sawa.

Kinachotakiwa ni kucheza kwa umakini na kila mmoja kuwa mlinzi wa mchezaji mwenzake kwa kuwa muda uliopo kwenye mashindano ya Mapinduzi kila mmoja anapaswa kufanya kazi yake hili ni muhimu.

Wachezaji wanatambua umuhimu wa kupata matokeo hivyo kinachotakiwa ni kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati ndani ya dakika 90.

Ikitokea matokeo yakakosekana haina maana kwamba itakuwa ni mwisho wa mchezo bado kuna wakati mwingine unakuja wachezaji watapata nafasi ya kurekebisha makosa.

Makosa yaliyopita kwenye mechi moja ni muhimu kufanyiwa kazi na hilo litafanya mwendelezo mzuri kupatikana kwa mechi zijazo na inawezekana.