INAELEZWA kuwa Klabu ya Yanga ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Medeama Jonathan Sowa.
Hiyo yote ni kwa ajili ya kuboresha eneo la ushambuliaji ambalo halijapata mbadala sahihi baada ya kusepa kwa Fiston Mayele.
Kasi ya Yanga kwa sasa kwenye ufungaji sio yakubeza lakini inaongozwa na viungo washambuliaji.
Ni Aziz KI huyu ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa katupia mabao 10 kama ilivyo namba ya jezi yake.
Taarifa zimeeleza kuwa Yanga ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota huyo kuongeza nguvu katika eneo hilo kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa.