WAZIRI NDUMBARO ATEUA KAMATI YA HAMASA KWA TIMU ZA TAIFA, BABA LEVO, JOTI, OSCAR OSCAR

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), ameteua Kamati Maalum kwa ajili ya hamasa kwa timu za Taifa zilizofuzu mashindano mbalimbali ya Kimataifa. Kamati hii inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu pamoja na Wajumbe 16.

Kamati hii itakuwa na jukumu la kuhamasisha washabiki na wapenzi wa michezo ndani na nje ya nchi kujitokeza kuzishangilia na kuziunga mkono timu za Taifa pamoja na kuratibu hafla maalum ya harambee ya kuzichangia timu za Taifa inayotarajiwa kufanyika tarehe 10 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hotel ya Johari Rotana ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya harambee hiyo.

Wajumbe wa Kamati walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

1. Theobald Sabi – Mwenyekiti,

2. Patric Kahemela – Makamu Mwenyekiti,

3. Neema Msitha – Katibu,

4. Beatrice Singano – Mjumbe,

5. Michael Nchimbi – Mjumbe,

6. Jemedari Said – Mjumbe,

7. Nick Reynolds (Bongo Zozo) – Mjumbe

8. Hamis Ali – Mjumbe,

9. Christina Mosha (Seven) – Mjumbe,

10. Mhandisi Hersi Said – Mjumbe,

11. Salum Abdallah (Try Again) – Mjumbe,

12. Paulo Makanza – Mjumbe,

13. Mohamed Soloka – Mjumbe,

14. Hassan Mohamed Raza – Mjumbe, ,

15. Lucas Mhavile (Joti) – Mjumbe

16. Oscar Oscar – (Mzee wa Kaliua) – Mjumbe,

17. Prisca Kishamba – Mjumbe,

18. Burton Mwemba (Mwijaku) – Mjumbe,

19. Clayton Revocatus Chipondo (Baba Levo) – Mjumbe.

Uteuzi wa Kamati hii unaanza kazi mara moja.