KWENYE mchezo wa pili wa Kombe la Mapinduzi 2024 Yanga wamezidi kupeta baada ya kupaa ushindi kwa mara nyingine tena.
Walianza na funga 2023 Desemba 31 ubao uliposoma Jamhuri 0-5 Yanga wakakomba pointi tatu na kete ya pili fungua Januri 2024 ilikuwa Januari 2 2024.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Jamus FC 1-2 Yanga zilikuwa dakika 90 zenye ushindani mwanzo mwisho ambapo pointi tatu zilikuwa mali ya Yanga.
Farid Mussa alifungua pazia la mabao dakika ya 16 liliwekwa usawa na David Clement dakika ya 42 akitumia makosa ya ulinzi ya Yanga walipoacha nafasi kwa kwenda mbele kutafuta bao lingine.
Nickson Kibabage jioni alifunga bao la ushindi dakika ya 90+7 akitumia pasi ya Clement Mzize.
Leo Januari 3 ni APR v JKU saa 10:15 kisha Simba SC v Singida Fountain Gate saa 2:15.