TAIFA STARS NDANI YA MISRI TAYARI KWA KAZI

JANUARI 2 2024 Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imewasili salama jijini Cairo, Misri kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujiandaa na Afcon 2023.

Mashindano hayo makubwa yanatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11 nchini Ivory Coast.

Taifa Stars   imepangwa kundi “F” ikiwa na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni mara ya tatu Stars kuwa ndani ya AFCON baada ya kufanya hivyo 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche amesema kuwa watakuja na mipango tofauti itakayowapa matokeo kwenye mechi zao kutokana na maandalizi.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Bacca, Feisal Salum, Dickson Job, Aishi Manula, Mudhathir Yahya.