BALEKE, NTIBANZOKIZA KUKUTANA NA BALAA HILI SIMBA

MASTAA wa Simba kwenye upande wa ushambuliaji ikiwa ni Jean Baleke, John Bocco na viungo Saido Ntibanzokiza watakutana na balaa la Kocha Mkuu, Abdlehak Benchikha kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo walizipata kwenye mechi dhidi ya KMC.

Desemba 23 ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa Simba ndani ya 2023 katika Ligi Kuu Bara walishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma KMC 2-2 Simba. Mabao ya Simba yalifungwa na Saido Ntibanzokiza na Jean Baleke huku Wazir Junior akifunga mabao yote kwa KMC.

Mara baada ya mchezo, Benchikha aliweka wazi kuwa walitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo huo lakini ilikuwa ni tatizo kwao kwenye upande wa kuzibadili nafasi hizo kuwa ushindi jambo ambalo watalifanyia kazi.

Tulitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wetu lakini tatizo kubwa ni kwamba tulishindwa kuzibadili kuwa mabao jambo ambalo tulikuwa tukilifanyia kazi kwenye mechi zilizopita na sasa tunakwenda kufanyia kazi hili.

“Ni tatizo kwetu hilo tunalitambua kwa uwa ili ushinde ni lazima ufunge sasa tutazungumza na wachezaji na kuona kwamba katika hili tunakuwa imara kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” .

Kwenye upande wa ushambuliaji ndani ya kikosi cha Simba ni Jean Baleke ni namba moja akiwa katupia mabao 8.