KLABU ya Azam FC inakwenda kufunga mwaka 2023 wakiwa ni namba moja kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Chini ya Kocha Mkuu Yusuph Dabo kikosi cha Azam FC kimekuwa kwenye mwendo wa dhahabu na kupata matokeo kwenye mechi walizokuwa wanacheza.
Mchezo wake wa mwisho ndani ya 2023 walikomba pointi tatu ugenini ilikuwa ni Desemba 21 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-4 Azam FC.
Katika mchezo huo nyota Feisal Salum alipachika bao moja linalomfanya afikishe jumla ya mabao 8 akiwa namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Azam FC.
Mechi 13 walizoshuka uwanjani ambazo ni dakika 1,170 walikomba ushindi kwenye mechi 10 ambazo ni dakika 10 wakipoteza mechi mbili ambazo ni dakika 180 na sare ni mchezo mmoja ndani ya dakika 90.
Kibindoni ina pointi 31 kwenye msako wa pointi 39 ilipishana nazo 8 huku safu ya ushambuliaji ikitupia jumla ya mabao 35 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 33.
Mabao ya kufungwa ni 10 kwenye upande wa ulinzi ikiwa na wastani wa kuokota bao moja kila baada ya dakika 117.