ABDELHAK Benchikha, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna ari kubwa kwa wachezaji wa timu hiyo katika kutimiza majukumu jambo ambalo linaongeza nguvu katika kutafuta matokeo uwanjani.
Simba inatarajiwa kukaribishwa na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Azam Complex, Desemba 23 ikiwa ni mzunguko wa kwanza.
Mchezo wa ligi uliopita ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma Simba 3-0 Kagera Sugar hivo kibarua kingine kinatarajiwa kuwa ugenini.
“Kila mchezaji anaonyesha ari ya kutafuta matokeo kikubwa ni kuona tunakuwa kwenye mwendo mzuri wa kupata ushindi.