KUTOKA Morogoro, Klabu ya Mtibwa Sugar haina bahati na Uwanja wa Azam Complex kwa msimu wa 2023/24 kutokana na kukwama kukomba pointi ndani ya dakika 180.
Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila ni mechi mbili tofauti ilicheza ikiwa ugeni ilikuwa ni Novemba 24, 2023 ubao uliposoma Azam FC 5-0 Mtibwa Sugar.
Dakika 180 zilikamilishwa Desemba 16, 2023, ubao ulisoma Yanga 4-1 Mtibwa Sugar. Katika mechi mbili ni mabao 9 timu hiyo ilitunguliwa huku safu ya ushambuliaji ikifunga bao moja pekee kupitia kwa Seif Karihe.
Msako wa pointi sita ugenini ilipishana nazo mazima kwa kuziacha zote kwenye uwanja huo katika mechi za ligi ambazo zilikuwa na ushindani mkubwa.
Kwenye msimamo Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi zake tano kibindoni.