GAMONDI AENDELEZA UBABE BONGO

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameendeleza ubabe wake kwa kushuhudia wachezaji wake wakiibuka na ushindi wa mabao 4-1 Mtibwa Sugar.

Kwenye mchezo uliochezwa Desemba 16 Uwanja wa Azam Complex, Yanga walipeta na kukomba pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar wakiendeleza ubabe wao kwenye ligi.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Aziz KI ambaye alifunga mabao mawili, Kenedy Musonda na Skudu Makudubela huku lile la Mtibwa Sugar likifungwa na Seif Karihe dakika ya 90.

Gamondi amesema furaha kubwa ni kwa vijana wake kupata ushindi kwenye mechi wanazocheza jambo ambalo linahitajika kuwa endelevu.