KAGERA YAIPIGIA HESABU KALI DODOMA JIJI

UONGOZI wa Kagera Sugar umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi kuu Bara unatarajiwa kupigwa  Oktoba 25, kwenye Dimba la Jamhuri mjini Dodoma.

Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamisi Mazanzala aliliambia Championi  Jumatano kuwa, maandalizi yapo sawa kwa ajili ya mchezo huo.

“Maandalizi yapo sawa na wachezaji wapo tayari kupambana kuona namna gani tutapata matokeo hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu sio timu ya kubeza.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini watambue kwamba tuna kikosi kipana, na mashabiki wetu hivyo kikubwa tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo, mashabiki wajitokeze kwa wingi,” alisema Mazanzala.