MSAFARA wa Simba uliokuwa na jumla ya wachezaji 24 umewasili salama Dar ukitokea Misri ulipokuwa kwa ajili ya mchezo wa African Football League.
Ni mapambano ya dakika 90 dhidi ya Waarabu wa Misri ilikuwa kwenye mchezo wa kuamua nani atakayetinga hatua ya nusu fainali kimataifa.
Oktoba 24, ubao ulisoma Al Ahly 1-1 Simba. Kwenye hatua ya robo fainali Simba wamegotea hapo kwa kuondolewa kikanuni.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-2 Al Ahly hivyo jumla inakuwa ni mabao 3-3, Al Ahly wanasonga mbele kwa faida ya mabao waliyoifunga Simba mchezo wa kwanza.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Israel Mwenda, Shomari Kapombe, Kennedy Juma, Onana Willy, Che Malone na John Bocco.