KUTOKANA na mwendo mgumu wa timu ya Namungo kupata matokeo kwenye mechi za ligi msim wa 2023/24 aliyekuwa kocha wa Namungo FC, Cedric Kaze ametangaza kung’atuka kwenye nafasi hiyo.
Taarifa yake ya kubwaga manyanga ndani ya Namungo inayotumia Uwanja wa Majaliwa kwenye mechi za ushindani aliitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
Kaze ameandika “leo nimeamua kujiuzulu kama Kocha Mkuu wa Namungo, ningependa kutumia fursa hii kuushukuru uongozi, watendaji wenzangu wa benchi la ufundi na wachezaji kwa ushirikiano na kujitoa kwao”
Kaze pia amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano wao. Mchezo wa mwisho Kaze kukaa benchi ilikuwa ni Oktoba 21 dhidi ya Singida Fountain Gate.